Trump: Ukraine ‘isahau’ kujiunga na NATO

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Ukraine “isahau” kujiunga na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO), tamko ambalo ni pigo kwa azma ya muda mrefu ya nchi hiyo ya Ulaya, ambayo iliungwa mkono na Rais wa zamani Joe Biden.