
Rais wa Marekani aliambia Fox News kwamba Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky “anafanya iwe vigumu sana kufikia makubaliano” ya kukomesha mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine. Rais wa Ukraine mwenyewe amesisitiza katika hotuba yake ya jioni umuhimu wa ushirikiano kati ya Ulaya na Marekani katika kufikia amani.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Donald Trump amesema siku ya Ijumaa, Februari 21, kwamba haoni kuwa ni muhimu kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuwepo katika mazungumzo yanayolenga kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine. “Sidhani kama ni muhimu sana kwa rais wa Ukraine kushiriki mkutano,” Trump amesema katika mahojiano ya sauti na Fox News. “Yuko mamlakani kwa miaka mitatu. Anafanya kuwa vigumu sana kufikia makubaliano.”
Baadaye, rais wa Marekani ameongeza kuwa viongozi wa Ukraine “hawana kadi yoyote” katika mazungumzo hayo. “Nimekuwa na mazungumzo mazuri sana na [Rais wa Urusi Vladimir Putin], na sijafanya mazungumzo hayo mazuri na Ukraine. Hawana kadi yoyote, lakini wanajaribu kuvuruga. Lakini hatutaacha hili liendelee,” Trump aliwaambia magavana wa Marekani katika Ikulu ya White House siku ya Ijumaa.
Kyiv na Ulaya zimelalamikia kutengwa kwa Ukraine baada ya Trump kufungua mazungumzo na Moscow kuhusu kumaliza vita hivyo vilivyoanza na mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine mwaka 2022. Wanadiplomasia wa Urusi na Marekani walikutana nchini Saudi Arabia mapema wiki hii kuzungumzia kuhusu kusitisha mapigano na Kyiv haikualikwa.
Nchi za Ulaya zataka kushawishi mazungumzo yajayo
Mvutano na Kyiv uliongezeka zaidi wakati rais wa Marekani kutoka chama cha Republican alipomtaja Zelensky kama “dikteta” na kudai kuwa Ukraine “imeanza” vita. “Analalamika kwamba hayuko katika mkutano ambao tunafanya na Saudi Arabia kujaribu kuleta amani ya kati,” Trump alisema katika mahojiano yake siku ya Ijumaa. “Alishiriki mikutano mbalimbali kwa miaka mitatu na hakuna kilichofanyika.”
Kwingineko katika hotuba hiyo, ambayo aliitoa baada ya misururu ya miito na viongozi wa nchi washirika, Zelensky alisema “Ulaya lazima na inaweza kufanya mengi zaidi ili kuhakikisha kuwa amani inapatikana” nchini Ukraine.
Aliongeza kuwa “inawezekana” kufikia mwisho wa vita na Urusi kwa vile Ukraine na washirika wake barani Ulaya wana “mapendekezo ya wazi.”
“Kwa msingi huu tunaweza kuhakikisha utekelezaji wa mkakati wa Ulaya, na ni muhimu kwamba hii inafanywa pamoja na Marekani,” alisema.
Trump, katika Ikulu ya White House Ijumaa kwa waandishi wa habari, alisema Putin na Zelensky watalazimika “kuungana” kumaliza vita.
“Nadhani Rais Putin na Rais Zelensky watalazimika kukutana. Kwa sababu unajua nini? Tunataka kuacha kuua mamilioni ya watu.”