Rais wa Ukraine, Volodymry Zelensky, amesema wamejadiliana na rais Donald Trump, kuhusu uwezekano wa Washington kuendesha kinu chake cha nishati ya nyuklia kilichopo Zaporizhizia, kusini mwa nchi hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Matamshi yake kwa waandishi wa habari, ameyatoa saa chache baada ya kuzungumza na rais Donald Trump, ambaye alimueleza nia ya nchi yake kusimamia shughuli za kinu hicho kama sehemu ya kupata makubaliano ya kusitisha mapigano na Urusi.
Zelensky amesema walizungumzia kinu kimoja tu, ambacho ndio kikubwa zaidi barani Ulaya kuzalisha nishati na kilidhibitiwa mwezi Februari mwaka 2022 na kimekuwa kitovu cha wasiwasi wa kutokea janga jingine la mionzi.
Aidha Zelensky ameongeza kuwa huenda ikachukua miaka miwili au zaidi kwa kinu hicho kuanza kufanya kazi kwa ufanisi kuzalisha umeme wa nchi yake na ule wa Mataifa ya Ulaya.
Trump na Zelensky wamezungumza siku chache kupita tangu Washington ikubaliane na Moscow kusitisha mashambulio ya miundombinu ya nishati kwa siku 30.