

Chanzo cha picha, LEON NEAL/GETTY IMAGES
Na Jess Parker and James Waterhouse
Kutoka Berlin and Kyiv
Je iwapo Donald Trump atakuwa rais wa Marekani kwa awamu nyengine kutakuwa na athari gani kwa Ulaya?
Viongozi wa Ulaya na mabalozi wanajiandaa kukabiliana na changamoto iwapo kutakuwa na mabadiliko utawala nchini Marekani.
Wakati Donald Trump alipomteua mbunge wa Ohio J.D Vance, ujumbe ulitumwa kwa Ulaya kuhusu jukumu lake kama Makamu wa rais.
Shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine, wasiwasi wa usalama na masuala ya biashara ni muhimu kwa Ulaya.
Hofu kubwa ya Ulaya kuhusu msimamo wa Trump utakuwa kuhusu masuala haya.
Katika mkutano wa usalama uliofanyika Munich nchini Ujerumani mwaka huu, alisema kwamba Ulaya inapaswa kujua kwamba Marekani iko makini kuhusu Asia Mashariki.
“Usalama wa Ulaya umedhoofishwa na sera za usalama za Marekani alisema.
Niels Schmid, ambaye ni mbunge mwandamizi kutoka chama cha Kansela wa Ujerumani Olaf Scholtz na mkuu wa sera za kigeni wa chama cha Social Democrats katika bunge la Ujerumani, ameiambia BBC kuwa Marekani itasalia katika NATO hata iwapo serikali ya Republican itaingia madarakani, hata kama Vance atachukua msimamo tofauti na Donald Trump.
Hata hivyo, ameonya kuwa vita vya kibiashara vitaanza chini ya uongozi wa Trump.
Kwa nini Ulaya inahofu?
Wanadiplomasia waandamizi katika Umoja wa Ulaya wanasema kuwa Trump amekuwa rais kwa miaka minne, hivyo hakuna mtu anayejidanganya.
Alisema, “Tunaelewa maana ya Trump kurudi madarakani. Haijalishi ni nani Makamu wa Rais aliye naye.”
Aliulinganisha Umoja wa Ulaya na meli inayojigamba kwa dhoruba na kusema kwa sharti la kutotajwa jina kwamba hatua zozote zitakazochukuliwa, hali iliyopo mbele itakuwa ngumu.
Marekani imekuwa mshirika mkubwa wa Ukraine iliyokumbwa na vita kwa miaka miwili iliyopita.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema wiki hii, “Siogopi Trump kuwa rais, natumaini tunaweza kufanya kazi pamoja.”
Zelensky pia anaamini kwamba viongozi wengi wa chama cha Republican na raia wako upande wa Ukraine.

Chanzo cha picha, @BORISJOHNSON
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson ni rafiki mzuri na Volodymyr Zelensky na Trump. Boris Johnson anaunga mkono msaada kwa Ukraine
Johnson alikutana na Trump katika mkutano wa kitaifa wa chama cha Republican.
Baada ya mkutano huo, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa “Trump atachukua maamuzi magumu na ya dhati kulinda uungwaji mkono wa nchi na demokrasia.”
“Hatuna uhusiano wowote na kile kinachotokea Ukraine,” alisema katika kipindi cha podcast siku chache kabla ya operesheni ya kijeshi dhidi ya Ukraine kuanza.
Vance alikuwa na jukumu muhimu katika msaada wa dola bilioni 60 za Marekani kwa Ukraine.
Je, jukumu la Trump litakuwa nini nchini Ukraine?
“Ni muhimu kwetu kujaribu kuwashawishi,” anasema Yevhen Mahda, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sera ya Dunia, taasisi ya sera iliyopo mjini Kyiv.
Alisema: “Serikali ya Trump ilihusika katika vita vya Iraq. Tunaweza kumualika Trump kuitembelea Ukraine ili aweze kujionea mwenyewe kile kinachoendelea huko. Pia ataweza kuona jinsi misaada ya fedha inayotolewa na Marekani inavyotumiwa huko.”
Itakuwa muhimu kwa Ukraine kuelewa ni ushawishi kiasi gani wanaoweza kuutumia kumshawishi rais mpya wa Marekani.
Mfuasi mkubwa wa Trump na Vance katika Umoja wa Ulaya ni Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán.
Orban hivi karibuni alikutana na Zelenskiy na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Baada ya hapo, alikutana na Trump nchini Marekani. Putin na Orban wana uhusiano mzuri.

Chanzo cha picha, @PM_VIKTORORBAN
Katika barua kwa Katibu mkuu wa Umoja wa Ulaya, Orban amesema iwapo Trump atashinda uchaguzi wa urais, hatasubiri hadi atakapokula kiapo na atataka makubaliano ya amani kati ya Urusi na Ukraine haraka iwezekanavyo.
“Wana mpango wa kina kuhusu hili.” Ameandika katika barua hiyo.
Wakati huo huo, Zelensky alisema wiki hii kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin anapaswa pia kuhudhuria mkutano wa amani uliopendekezwa mnamo Novemba mwaka huu.
Alisema kuwa atakuwa na mpango kamili tayari mwezi Novemba. Lakini pia alifafanua kuwa hakuna shinikizo kutoka kwa nchi za magharibi dhidi yake.

Chanzo cha picha, SAMUEL CORUM/AFP VIA GETTY IMAGES
Oraban hivi karibuni alitembelea Urusi na China kama sehemu ya ujumbe wa amani. Alishtumiwa kwa kutumia vibaya urais wa baraza hilo ambalo alilishikilia kwa miezi sita.
Kutokana na vitendo vya Orban, maafisa wa Tume ya Ulaya walisema hapaswi kuhudhuria mikutano huko Hungary.
Mwaka huu, Hungary imepata urais wa Baraza la Ulaya kwa miezi sita. Baada ya hapo Orban ametembelea, Ukraine, Azerbaijan, China na Marekani.
Wasiwasi kuhusu mustakabali wa kibiashara
Wakati wa utawala wa Donald Trump, vikwazo viliwekwa kwa bidhaa za chuma na aluminium kutoka Umoja wa Ulaya.
Baada ya hapo, Joe Biden, ambaye aliingia madarakani, alipiga marufuku kodi hii ya uagizaji. Trump amependekeza kodi ya asilimia 10 kwa bidhaa zote zinazoingizwa nchini Marekani iwapo atachaguliwa.
Kwa upande wa biashara, mgogoro wa kiuchumi na Marekani utaonekana kama athari mbaya katika sehemu kubwa ya Ulaya.
“Kitu kimoja tunachojua kwa hakika ni kwamba kutakuwa na hatua za adhabu dhidi ya Umoja wa Ulaya na tunapaswa kujiandaa kwa vita vya biashara,” anasema Nils Schmid, mkuu wa sera za kigeni wa chama cha Social Democrats katika bunge la Ujerumani.
Awali, Vance alikuwa ameikosoa Ujerumani juu ya suala la kijeshi.
Haikuwa nia yake kuikosoa Ujerumani. Alisema kuwa viwanda vya kutengeneza silaha havipati msaada wa kutosha.
Baada ya ‘kampeni ya kijeshi’ ya Urusi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholtz alilitaja tukio hilo la kihistoria katika hotuba yake kwa bunge.
Katika hotuba yake bungeni baada ya shambulio la Ukraine, alianzisha marufuku ya usafirishaji wa silaha nje ya nchi. Pia alitoa maoni juu ya kuongeza kwa matumizi ya usalama wa nchi na kupiga marufuku ununuzi wa mafuta na gesi kutoka Urusi.
Ujerumani inasema ni ya pili kwa Marekani katika kuisaidia Ukraine.

Chanzo cha picha, MARYAM MAJD/GETTY IMAGES
Kwa mara ya kwanza tangu vita baridi, Ujerumani imeweza kutenga asilimia mbili kwa ajili ya vikosi vya ulinzi, licha ya kwamba ni bajeti ya muda mfupi.
“Nadhani tuko kwenye njia sahihi,” anasema Nils Schimd. Tunataka kujenga upya jeshi. Haijawahi kuangaliwa kwa miaka 15 hadi 20. Wale wanaofuatilia hatua hizi za Ujerumani hawakubaliani kwamba maandalizi ya nyuma ya matukio ni makubwa au ya kutosha.”
Viongozi wenye utashi wa kisiasa wa kupata na kuimarisha mustakabali wa bara la Ulaya ni wachache na hawapatikani.
Olaf Scholtz ana mbinu tofauti ya wastani na anaepuka kuitumia.
Katika ngazi ya kisiasa, anakabiliwa na matatizo mengi na anaweza kutokuwa mamlakani katika uchaguzi ujao.
Rais Macron wa Ufaransa ametangaza uchaguzi mdogo na hali yake imekuwa mbaya tangu wakati huo.
Nchini kwake watu wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia hawakupata uongozi kama ilivyotarajiwa. Kwa hiyo, kuna aina fulani ya kupooza kisiasa.
Rais wa Poland Andrzej Duda alionya Jumanne (Julai 16) kwamba ikiwa Urusi itapoteza vita dhidi ya Ukraine, uwezekano wa vita na nchi za Magharibi unaweza kuongezeka.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi