Trump atoa wito wa watu kuhama Tehran, Iran yaahidi mashambulizi dhidi ya Israel hadi alfajiri

Siku nne baada ya kuanza kwa mashambulizi makubwa ya Israeli dhidi ya Iran, mzozo kati ya nchi hizo mbili hauonyeshi dalili ya kupungua, huku msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran akitangaza mashambulizi dhidi ya Israeli yataendelea hadi asubuhi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Marekani Fox News, Rais wa Marekani Donald Trump ameomba Baraza la Usalama la Taifa lijiandae kwa mgogoro mkubwa kabla ya kurejea mapema kutoka mkutano wa G7 nchini Canada. Donald Trump amekatisha ziara yake kwenye mkutano na anarejea Washington. Amezungumzia hali ya Mashariki ya Kati, na tangazo hili limekuja saa chache baada ya Donald Trump kutangaza kwamba “kila mtu anapaswa kuondoka mara moja Tehran.”

Vikosi vya Marekani vimesalia “katika mkao wa kujihami” katika Mashariki ya Kati

Vikosi vya Marekani “viko katika mkao wa kujihami” katika Mashariki ya Kati, “na hilo halijabadilika,” msemaji wa Ikulu ya Marekani Alex Pfeiffer amesema siku ya Jumatatu kwenye mtandao wa kijamii wa X. “Tutatetea maslahi ya Marekani” katika eneo hilo, ameongeza, wakati mzozo kati ya Israeli na Iran ukiendelea kwa usiku wa tano mfululizo.

Wakati huo huo jeshi la Israeli linadai kuwa limenasa ndege kadhaa zisizo na rubani zilizorushwa kuelekea Israeli katika muda wa saa moja iliyopita. Ndege zilifyatua ving’ora katika maeneo ya Ramat Magshimim na Haspin, katika eneo la kusini la milima la Golan linalokaliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *