
Umoja wa mataifa unamtaka rais wa Marekani, Donald Trump, kutotekeleza sheria ya kuongeza ushuru kwa bidhaa kutoka mataifa yanayoendelea, UN ikisema hilo litakuwa athari hasi kwa mataifa husika.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matangazo ya kibiashara
UN kupitia kitengo chake cha biashara, Unctad, imesema hatua ya rais Trump kutangaza kuongeza ushuru wa asilimia 10 haufai kwani mataifa hayo hayana uwezo wa kushindana na Marekani kiuchumi, kwani ni madogo.
Mataifa yanayotarajiwa kuathirika zaidi na tangazo la rais Trump ni pamoja na Laos linalopatikana kusini mwa Asia ambalo limetangaziwa ushuru wa asalimia 48, Mauritius asilimia 40 na Myanmar ushuru wa asailimia 45, mengine yakiwa ni Malawi na Msumbiji.
Rais Trump amenukuliwa akisema hatua yake inatokana na ushindani wa biashara usiofaa kutoka kwa washindani wa Marekani, ambao wamekuwa wakichukua hatua kali za kibashara dhidi ya Marekani, hivyo Marekani ikitakiwa kujibu hatua hizo.