Trump arudia kutamka bila ya aibu kuwa amejitolea ‘kuinunua Ghaza na kuifanya milki’ ya Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amerudia tena kutamka bila aibu pendekezo lake tata la kulinyakua na kulidhibiti eneo la Ukanda wa Ghaza, akisema amejitolea “kulinunua na kulimiliki” eneo hilo lililoharibiwa na vita.