Trump aiwekea vikwazo mahakama ya kimataifa ya uhalifu na kuitaja kuwa ”si halali”

Rais Donald Trump ametia saini amri ya utendaji inayoiwekea vikwazo mahakama ya kimataifa ya uhalifu, akiituhumu kwa “vitendo vinavyokiuka sheria na visivyo na msingi vinavyoilenga Marekani na mshirika wetu wa karibu Israel”.