Trump aapa kuweka hadharani nyaraka za siri za mauaji ya kina Kennedy na Martin Luther King Jr.

Rais mpya wa Marekani Donald Trump ameahidi kuweka hadharani nyaraka za serikali zilizoainishwa kuwa za siri zaidi, zinazohusiana na mauaji ya Rais John F. Kennedy, Seneta Robert F. Kennedy, na mwanaharakati wa haki za kiraia Martin Luther King Jr.