TRC yapata hasara ya Sh224 bilioni

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa Tanzania, Charles Kichere amesema mwaka wa fedha 2023/2024, Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilipata hasara ya Sh224 bilioni ikilinganishwa na Sh102 bilioni mwaka uliopita.

CAG Kichere amesema hasara hiyo imechangiwa na kupungua kwa mapato ya usafirishaji kutokana na uhaba wa vichwa vya treni na mabehewa pamoja na mvua kubwa iliyosababishwa kufungwa kwa njia kwa miezi minne.

Kichere ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 27, 2025 wakati akiwasilisha ripoti yake ya mwaka 2023/2024 kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Shirika lilitumia kiasi cha Sh29 bilioni ikiwa ni ruzuku kutoka serikalini kama ruzuku hilo isingetolewa shirika lingepata hasara ya Sh253 bilioni.

Kichere amesema taarifa hiyo haihusu mapato ya SGR kwa sababu taarifa inaishia Juni 30, 2024 ambapo treni ilikuwa haijaanza.

Amependekeza shirika lijikite katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wake pamoja na kutekeleza hatua za kupunguza gharama na mpango wa kina kupata injini na mabehewa ili kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *