Na Issa Mwadangala
ACP Akama alisema, wakati wakielekea kwenye sherehe hiyo inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, wamejipanga kupata elimu pamoja na kuwafariji wahitaji katika jamii.
“Jeshi la Polisi hasa Askari wanawake hatuna budi kulifanya hili ili kuendelea kujenga ukaribu kati yetu na jamii kwa lengo la kupata taarifa za uhalifu na kuzishughulikia pindi tuzipatazo na jamii iendelee kuwa salama” alisema ACP Akama.
Katika kikao hicho alielezea umuhimu wa siku hiyo ambayo inalenga kuunga mkono harakati zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kumuwezesha mwanamke kwenye nafasi za uongozi, uchumi na maamuzi.
The post TPF Net GALA YAPAMBA MOTO-SONGWE appeared first on Mzalendo.