Tovuti ya RFIKISWAHILI kuwa na muonekano mpya kuanzia June 6

Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International, Jumatatu ya wiki ijayo, June 6 itazindua rasmi muonekano mpya wa tovuti yake ya kiswahili, ambao sasa wasikilizaji wataweza kupata vitu vingi na vipya kwa wakati mmoja. 

Imechapishwa: Imehaririwa:

Matangazo ya kibiashara

Kwa zaidi ya miaka mitano sasa toka kuanza kurushwa kwa matangazo ya kiswahili ya idhaa hii kutokea studio zetu za Dar es Salaam, Tanzania, tovuti yetu imekuwa mstari wa mbele kuchapisha habari muhimu, za uhakika na kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kusikiliza matangazo yetu ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao.

Mabadiliko haya ya tovuti yetu ni kwaajili ya kwenda na wakati uliopo ili kutoa nafasi zaidi kwa wanaotembelea mtandao wetu kwaajili ya kusoma, kupakua na kusikiliza matangazo yetu kwa lugha ya kiswahili.

Kupitia tovuti yetu mpya, taarifa zetu zinarahisishwa zaidi ambapo sasa utaweza kuutumia kwa kutumia simu yako ya Iphone, Android, Window Phone, Tablet na Ipad.

Kupitia simu yako ya kiganjani, utaweza kuperuzi tovuti yetu kwa urahisi zaidi, ikiwa ni pamoja na kusikiliza matangazo yetu ya moja kwa moja kwa kiswahili na lugha nyingine.

Kuanzia Jumatatu ya June 6, msikilizaji wa RFIKiswahili, kama unatumia simu ya kiganjani utatakiwa kutapakua “Download” programu maalumu ya RFIKiswahili na kuihifadhi kwenye simu yako tayari kwa kuanza kuitumia.

Kwa wanaotumia kompyuta “Desktop” hautapaswa kupakua “Download” programu ya RFIKiswahili zaidi ya kukubali kutumia “Cookies” za mtandao wetu ili kukurahisishia kufungua kurasa mbalimbali kupitia tovuti yetu na kwa haraka.

Muonekano huu mpya unavutia na ni rahisi kuperuzi.