
Kwa mara ya kwanza, siku ya Jumamosi Februari 15, maseneta 41 kati ya 61 wanatarajiwa kuchaguliwa na madiwani wa manispaa. Ishirini waliosalia watateuliwa na Rais wa Jamhuri, Faure Gnassingbé. Uchaguzi uliyo na masuala makuu ambayo yanathaminiwa tofauti na wanasiasa wa Togo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Lomé, Peter Sassou Dogbé
Hii ni hatua muhimu katika uanzishwaji wa taasisi za Katiba mpya iliyotangazwa tarehe 6 Mei, 2024, ambayo ilmeifanya Togo kuingia katika Jamhuri ya 5.
Changamoto ya uchhaguzi huu wa maseneta: kuimarishwa kwa demokrasia, kulingana na mwalimu-mtafiti katika Chuo Kikuu cha Kara. Wagombea 89 wamejitokeza kuwania nafasi 41 zitakazojazwa leo Jumamosi na madiwani wa manispaa na madiwani wa mikoa. Viti vingine 20 vya Bunge la Seneti vitashikiliwa na maseneta watakaoteuliwa na Rais wa Jamhuri Faure Gnassingbé.
Mtaalamu wa masuala ya siasa nchini Togo Madi Djabakaté, anasema uhaguzi huu wa maseneta unathibitisha “mkakati wa serikali unaolenga kukamilisha uanzishwaji wa taasisi mpya katika mfumo unaodhibitiwa kikamilifu.”
Sehemu ya upinzani haitashiriki katika uchaguzi huu wa maseneta, kama vile Muungano wa Kitaifa wa Mabadiliko, Vikosi vya Kidemokrasia vya Jamhuri au Mienendo ya Wananchi walio Wengi. Kila mtu anashtumu mchakato huu na anaona ni njia ya mkuu wa nchi kusalia madarakani kwa muda usiojulikana, wakati Katiba ya zamani ilimruhusu tu kugombea muhula mmoja wa mwisho mnamo 2025.
Kwa upande mwingine, chama cha Democratic Alliance for Integral Development na baadhi ya vyama vidogo vya upinzani viko kwenye kinyang’anyiro hicho sambamba na chama tawala cha Muungano kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano.