Togo: Faure Gnassingbé Rais wa Baraza chini ya katiba mpya

Nchini Togo, awamu ya mwisho ya utekelezaji wa Jamhuri ya Tano inaendelea, mwaka mmoja baada ya kutangazwa kwa Katiba mpya Mei 6, 2024. Jana usiku, serikali iliwasilisha barua yake ya kujiuzulu, ambayo ilikubaliwa na Rais Faure Gnassingbe, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari. Mnamo Mei 3, wabunge wanaitwa kumteua rais wa baraza, ambaye atakuwa na mamlaka ya utendaji. Kwa pamoja na maseneta, watachagua Rais wa Jamhuri mwenye jukumu la heshima.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Togo inakamilisha mpito wake kwa mfumo wa bunge, na kusitisha uchaguzi wa urais kwa upigaji kura wa moja kwa moja kwa wote. Mageuzi ambayo bado yanapingwa vikali na sehemu ya upinzani na mashirika ya kiraia.

Hatua ya kwanza, leo Jumamosi, Mei 3 asubuhi: Wabunge wa Togo wanaitwa kumteua rais wa baraza hilo. Kama mkuu wa serikali na majeshi, ana mamlaka ya utendaji chini ya katiba mpya. Jukumu hili ni la kiongozi wa chama kilicho wengi katika Bunge, yaani kwa mkuu wa nchi, Faure Gnassingbe, ambaye ameongoza nchi tangu mwaka 2005.

Uchaguzi wa wabunge wa mwaka jana ulikipa chama chake cha UNIR viti 108 kati ya 113 kwa muhula wa miaka sita. Matokeo bado yanapingwa na vyama kadhaa vya upinzani na mashirika ya kiraia.

Kuapishwa

Rais mpya wa Baraza kisha ataapishwa mbele ya Mahakama ya Katiba. Alasiri ya Mei 3, wabunge na maseneta watakutana katika kikao cha pamoja. Watamchagua rais mpya wa Jamhuri kwa kipindi cha miaka 4. Shughuli ambayo kimsingi imekuwa ya heshima.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Tano, anateua mabalozi, anatoa tuzo, na kumpokea Rais wa Baraza ili ajulishwe hali ya taifa. Kwa upande wao, baadhi ya wapinzani wanapanga kuhamasishana Mei 4 kwa ajili ya mkutano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *