Togo: Faure Gnassingbé aapishwa kama Rais wa Baraza

Togo imeingia katika Jamhuri ya Tano. Hatua mpya imefanyika Jumamosi hii, Mei 3, kwa kuapishwa kwa Faure Gnassingbé kwa wadhifa wa Rais wa Baraza, nafasi iliyoundwa kufuatia mabadiliko ya katiba mwaka wa 2024. Rais huyo wa zamani atabaki na mamlaka mengi ya utendaji.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Lomé, Peter Dogbé

Akiwa ameinua mkono wake wa kulia mbele ya meza ambayo kitabu cha Katiba kimewekwa, Faure Gnassingbe ametangaza fomula ya kiapo cha Kifungu cha 47 cha Katiba. Rais mpya wa Baraza  aliteuliwa mapema kidogo na Bunge.

Nje, mbele ya ikulu ya rais, wafuasi wa utawala walishikilia mabango yaliyoandikwa: “Sote kwa Togo yenye nguvu” na “Togo ina nguvu ikiongozwa na Faure.” Sherehe ya kuapishwa imemalizika kwa gwaride la kijeshi.

Faure Gnassingbé alimrithi babake, Gnassingbé Eyadéma, aliyefariki mwezi wa Februari 2005 baada ya kutawala kwa miaka 38. Muhula wake wa nne unatarajiwa kumalizika Mei 3. Atakuwa na umri wa miaka 59 mwezi Juni. Leo Jumamosi alasiri, wabunge na maseneta walikutana katika kikao cha pamoja kumchagua Rais mpya wa Jamhuri, kwa muhula wa miaka minne, nafasi ambayo sasa ni ya heshima. Kwa hivyo nchi inakamilisha mpito wake kwa utawala wa bunge ambao unafuta uchaguzi wa urais kwa upigaji kura wa moja kwa moja kwa wote, mageuzi ambayo bado yanapingwa vikali na sehemu za upinzani na mashirika ya kiraia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *