Timu ya Trump yakutana kwa siri na wapinzani wa rais wa Ukraine

Marekani inaendelea kuishinikiza serikali ya Ukraine ili ikubali kukabidhi utajiri wake wa madini ya kipekee mikononi mwa viongozi wa White House na sasa timu ya Donald Trump imekutana kwa siri na wapinzani wa rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy.