TIMU 20 ZA VIJANA MIKOA MITATU ZAPAMBANA MIRERANI 

Na Mwandishi wetu, Mirerani
TIMU 20 za vijana za soka za mikoa mitatu zimeshiriki bonanza lililofanyika kwenye viwanja vya Tanzanite Complex kwa Mnyalu uliopo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Timu hizo za vijana waliopo chini ya umri wa miaka 20, 17, 15, 13 na 11 ambao wametoka kwenye mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Tanzanite Complex Charles Mnyalu amesema lengo la bonanza hilo ni kukuza vipaji kwa vijana mbalimbali wa mikoa hiyo walioshiriki.
“Kupitia bonanza hili vijana wengi wamechaguliwa na maskauti mbalimbali wakiwemo wa shirikisho la soka nchini (TFF) na vipaji vyao vinaonekana,” amesema Mnyalu.
Amesema kupitia vipaji vyao baadhi ya vijana wamepata bahati ya kuchaguliwa kujiunga na timu kubwa ikiwemo timu za Taifa za vijana.
Amesema kwamba katika michuano hiyo mbali na zawadi tofauti wachezaji wa timu zitakazoshinda bonanza hilo watapatiwa kombe na medali.

The post TIMU 20 ZA VIJANA MIKOA MITATU ZAPAMBANA MIRERANI  appeared first on Mzalendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *