The Economist: Ukraine inahitaji muda wa karne kadhaa kuweza kulipa deni la fedha kwa Marekani

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na gazeti la The Economist linalochapishwa nchini Uingereza, ikiwa Ukraine itatia saini makubaliano na Marekani ya kulipa fidia ya dola bilioni 500, kwa kuzingatia kasi yake ya sasa ya ukuaji wa uchumi, itahitaji mamia ya miaka ili kuweza kulipa deni lake hilo.