
Utawala wa kijeshi nchini Burma umetangaza wiki ya moja ya maombolezo ya kitaifa Jumatatu, Machi 31, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi siku ya Ijumaa lililoua zaidi ya watu 1,700 nchini humo na nchi jirani ya Thailand.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kipindi cha maombolezo kinaendelea hadi Jumapili, wanajeshi walio madarakani wamesema katika taarifa, na kutangaza kushushwa kwa bendera za Burma hadi nusu mlingoti, linaripoti shirika la habari la AFP.
Maelfu ya watu wengine wamejeruhiwa nchini Mynmar kufuatia tetemeko hilo la ardhi, huku mamia wakiwa bado wamekwama kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Hata hivyo matumaini ya kupata watu walionusurika kwenye vifusi yamefifia Jumatatu, Machi 31, siku tatu baada ya tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 kuua zaidi ya watu 1,700 nchini Myanmar na Thailand.
Wakati zoezi la utafutaji likiendelea, lakini matumaini ya kupata manusura yanafifia, idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Myanmar inaweza kuwa kubwa zaidi.
Huko Mandalay, mji wa pili wa Myanmar, ulio karibu na kitovu cha tetemeko hilo, juhudi za kutoa msaada zimepungua siku ya Jumatatu asubuhi ikilinganishwa na siku iliyotangulia. Joto linapofikia nyuzi joto 40, hali ya kitropiki pia inatatiza kazi ya uokoaji na utambuzi wa miili.
Tetemeko hilo la ardhi liliharibu majengo, na barabara katika majimbo mbalimbali huku uongozi wa kijeshi akiomba msaada wa nchi mbalimbali kuwasaidia watu wake.