Televisheni ya Sudan: Jeshi liko karibu kuchukua udhibiti wa Ikulu ya rais kutoka kwa RSF

Televisheni ya taifa ya Sudani imesema siku ya Alhamisi kwamba jeshi linakaribia kuchukua udhibiti wa Ikulu ya rais mjini Khartoum kutoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), na hivyo kuashiria mabadiliko makubwa katika mzozo wa miaka miwili ambao unatishia nchi hiyo kusambaratika.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano jioni, mapigano makali yalizuka karibu na ikulu, huku milipuko ikisikika na mashambulizi ya anga ya jeshi yakilenga katikati mwa Khartoum, mashahidi na vyanzo vya kijeshi vimeliambia shirika la habari la REUTERS.

Baada ya takriban miaka miwili ya vita, RSF inadhibiti sehemu kubwa ya magharibi mwa Sudani na sehemu za mji mkuu Khartoum, lakini imekuwa ikipoteza maeneo kadhaa katikati mwa Sudani baada ya jeshi kuyarejesha chini ya himaya yake.

Makundi hayo mawili ya kijeshi yalifanya mapinduzi mwaka wa 2021, yakiondoa mpito kwa utawala wa kiraia, na vita vilizuka mwezi Aprili 2023 baada ya mipango ya mpito mpya kuzua mzozo mkali.

Vita hivyo vimesababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita mzozo mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani, huku RSF na jeshi wakituhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *