
Kampuni ya michezo ya kubashiri, BetPawa, imetangaza udhamini wa Sh194 milioni kwa Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (NBL) inayoendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) ambayo inafanyika mkoani Dodoma.
Ofisa Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo, Ntoudi Mouyelo amesema wameamua kudhamini mpira wa kikapu nchini ili kusaidia kuukuza mchezo huo ambapo Sh130 milioni zimetengwa kwa ajili ya ‘Locker Room Bonus’ na Sh14 milioni kwa zawadi za ushindi na fedha zinazobaki zitasaidia usimamizi wa TBF.
“Kampuni yetu imejizatiti katika kukuza mchezo pamoja na kusaidia jamii,” alibainisha Mouyelo huku akifafanua kwamba ‘Locker Room Bonus’ katika NBL, ni mfumo wa zawadi kwa wachezaji 12 na maafisa wanne wa timu inayoshinda watakabidhiwa Sh140,000 kila mmoja.
Mbali na Locker Room Bonuses, kampuni hiyo pia imejitolea Sh14 milioni kugawanywa kwa wachezaji bora na timu itakayoshinda mwishoni mwa msimu wa 2025 huku kampuni hiyo ikiahidi kuwasadia mabingwa wa NBL katika Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika inayofuata.
“Tunalenga kuukuza mpira wa kikapu katika kanda hii, kama tulivyofanya Rwanda kupitia ushirikiano kama huu