
Hezbollah ilirusha msururu wa maroketi kutoka Lebanon usiku kucha, na kutua ndani zaidi ya Israel kuliko mashambulizi ya awali.
Majengo ya makazi huko Kiryat Bialik yamechomwa moto na baadhi ya watu kujeruhiwa. Vikosi vya uokoaji vilifika eneo la tukio kuwatibu majeruhi, huku vikosi vya usalama vya Israel vikizingira eneo hilo.