Tarabelsi: Juhudi za UN ni muhimu kwa ajili ya kuwarejesha makwao kwa hiari wahamiaji

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya, Emad al-Tarabelsi amesisitizia umuhimu wa kuweko msaada wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) katika kuendeleza jitihada za kuhakikisha wahamiaji wanaondoka Libya kwa hiari yake na kurejea kwenye nchi zao.