Tanzania: Watumiaji wa mtandao wa X wahangaika baada ya kufungwa

Nchini Tanzania, watumiaji wa mtandao wa X zamani Twitter bado wanahangaika kupata huduma za mtandao huo baada ya serikali kuripotiwa kuufunga.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo tulivyozungumza navyo, hadi tukichapisha taarifa hii, mtandao huo ulikuwa bado haujarejeshwa, baadhi wakilazimika kutumia VPN kuingia X.

Hapo jana, taasisi kadhaa za uma ziliripoti mitandao yake ya kijamii kudukuliwa, ambapo katika ukurasa wa X wa jeshi la polisi nchini humo, wadukuaji walichapisha ujumbe wa kupotosha kuhusu kifo cha rais.

Aidha kurasa kadhaa za viongozi, taasisi za uma kama jeshi la polisi na mamlaka ya mapato TRA, zilithibitisha kurasa zake za YouTube na X kudukuliwa.

Polisi nchini humo wanasema inawasaka watu waliohusika na udukuaji huo, ambao ndio ulipelekea kuzuiwa kwa muda kwa mtandao wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *