
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imewahukumu kifungo cha maisha jela watuhumiwa wanne kwa kesi ya ubakaji na ulawiti kwa kundidhidi ya binti wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam
Nje ya Mahakama hiyo wakili anayetetea watuhumiwa , Godfrey Wasonga amesema hawakuridhishwa na hukumu hiyo kwani kuna baadhi ya vifungu vimekiukwa.
Hata hivyo,licha ya wanne hao kuhukumiwa,pia wametakiwa kulipa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila mmoja kwa muathiriwa wa tukio hilo.