
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kimelaani kitendo cha kukamatwa kwa wanachama wake kumi na watatu na kutawanywa kwa vurugu kwa wafuasi wake siku ya Alhamisi karibu na mahakama ya Dar es Salaam, ambapo kiongozi wa chama hicho, Tundu Lissu, alitakiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhaini.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Rais wa chama hicho anakabiliwa na adhabu ya kifo kwa kosa hilo, wakati chama chake cha siasa hakitashiriki kwenye uchaguzi ujao wa mwezi Oktoba 2025 kwa kutotia saini kanuni mpya ya maadili ya uchaguzi, jambo ambalo Chadema inapinga.
Wafuasi wa chama hicho wanakemea vitendo vya ubabe vinavyofanywa na serikali ya Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania na mbinu za Chama Cha Mapinzi (CCM) kutaka kusalia madarakani.
Mamia ya watu walikusanyika karibu na mahakama ya Dar es Salaam nchini Tanzania siku ya Alhamisi, Aprili 24, huku njia ya kuingia kwenye jengo lenyewe ikizuiwa na idadi kubwa ya maafisa wa polisi. Wafuasi na viongozi wa chama cha Chadema walikamatwa na kupigwa walipokuwa wakijaribu kufika katika chumba ambacho kesi hiyo ingelisikilizwa.
Kumi na tatu wakamatwa
Kwa jumla, maafisa kumi na watatu wa kisiasa walikamatwa, akiwemo makamu wa rais na katibu mkuu. Chama hicho kinadai kuwa tisa kati yao walipelekwa msituni ambapo mwili wa mpinzani mmoja wa chama hicho ulipatikana mwezi Septemba mwaka jana. Chadema inadai mtu aliyejeruhiwa vibaya kichwani na polisi alifariki dunia.
Kukataa kuripoti mahakamani
Kutokana na hali hiyo, kiongozi wa upinzani Tundu Lissu ambaye alikamatwa Aprili 9, 2025 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, alikataa kufika mahakamani jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi hii. Tangu kukamatwa kwake, Chadema imelaani matatizo yanayowakabili ndugu zake na wanasheria wake katika kumtembelea.