Tanzania: Tundu Lissu kusikilizwa leo katika kesi ya uhaini inayomkabili

Kiongozi wa upinani nchini Tanzania Tundu Lissu anatarajiwa kusikilizwa leo Jumatatu katika kesi ya uhaini inayomkabili katika mahakam a ya Hakimu Mkaze Kisutu jijini Dar es Salaam. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Tanzania imetangaza kwamba mwenendo wote wa mashauri hayo utarushwa mubashara kwa umma kupitia mitandao rasmi ya Mahakama, kuwawezesha wananchi kuweza kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani kwa sababu Mahakama ya Kisutu inao uwezo wa kuchukua watu 80 pekee. 

Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Tundu Lissu alitiwa hatiani kwa kudai marekebisho katika mifumo ya uchaguzi nchini Tanzania.

Chama cha CHADEMA  kimeondolewa kwenye uchaguzi wa urais na ubunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Itakumlbukwa kwamba siku ya Ijumaa Mei 30, 2025 mawakili wa Kiongozi huyo wa upinzani waliwasilisha malalamiko yao kwa Jopo Kazi la Umoja wa Mataifa wakipinga kuendelea kushikiliwa kwake katika jitihada za kuongeza shinikizo la kimataifa la kutaka aachiwe huru, linaripoti shirika la habari la Uingereza Reuters.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *