
Takriban watu 28 walifariki Jumamosi, Juni 7, katika mojawapo ya ajali mbaya zaidi za barabarani katika miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania, mamlaka imetangaza siku ya Jumapili Juni 8, 2025.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Breki za lori zilifeli, na kusababisha kugongana na magari mawili, likiwemo basi dogo, na kutumbukia mtoni kusini magharibi mwa nchi hiyo, karibu na mpaka na Zambia, kamanda wa polisi wa eneo hilo Benjamin Kuzaga amesema katika taarifa yake.
Wahasiriwa 28 ni pamoja na wanawake 10 na watoto wanne, ameongeza, akihusisha ajali hiyo kutokana na “uzembe” wa dereva wa lori, “ambaye alishindwa kulidhibiti gari lake kwenye mlima mkali wa Iwambi.” Rais Samia Suluhu Hassan, katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X, ametoa rambirambi zake kwa familia za wahanga.
Tanzania inakumbwa na ajali mbaya za barabarani mara kwa mara.