
KATIKA uwanja wa Sokoine, Mbeya Kengold FC ambao wanaburuza mkia wakiwa na pointi 16 watakuwa na mtihani mgumu dhidi ya Tanzania Prisons, walioko nafasi moja juu yao wakiwa na pointi 21.
Kitakwimu kama KenGold itakubali kupoteza mchezo huo huenda ikawa imeshuka daraja kwani hesabu za vidole zitakazosalia si rafiki kwao.
Kumbukumbu za misimu mitatu nyuma zinaonyesha kwamba timu yoyote iliyoshindwa kufikisha pointi 30 ilishuka moja kwa moja. KenGold wasipoishinda Prisons hawawezi kufikisha pointi 30.
Baada ya mechi hii KenGold itabakiwa na michezo minne dhidi ya Coastal Union na Namungo ugenini na Pamba na Simba nyumbani.
Mchezo huo unakuja huku Kengold ikiwa kwenye hali mbaya zaidi baada ya kuchapwa mechi mbili mfululizo dhidi ya Azam FC (2-0) na Dodoma Jiji (3-0), hali iliyowaweka kwenye presha kubwa ya matokeo.
Prisons na wenyewe hawako salama kimahesabu kwani wanalazimika kupata pointi muhimu ingawa bado wanapumua kuliko majirani zao.
Kocha wa KenGold, Omary Kapilima, anakabiliwa na presha ya kusaka ushindi wa lazima nyumbani kwani wapinzani wao Tanzania Prisons wanakuja na morali ya ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya Kagera Sugar, huku kocha wao Amani Josiah akikiri