
Nchini Tanzania, polisi wameripotiwa kuzingira makaazi ya Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini na uchochezi na yale ya Makamu wake John Heche.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wakati hayo yakijiri kesi inayomkabili Lissu iliendelea tena siku ya Jumatatu, kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Kesi ambayo imekuwa ikiendelea ni kuhusu pingamizi wa Mawakili wa Lisu, kuhusu kesi hiyo kusikilizwa kwa njia ya mtandao, leo imekuwa ni fursa ya upande wa serikali kujitetea.
Awali, Polisi walionekana wakipiga doria katika maeneo ya Mahakama hiyo, huku waliojaribu kufika wakizuiwa. Wiki iliyopita, wafuasi wa chama hicho walikamatwa na wengine kupigwa na maafisa wa usalama baada ya kufika Mahakamani, kwa kukaidi onyo la polisi kutofika na kusisitiza kuwa wanalinda amani.
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, aliandika kuwa polisi walikuwa wamezingira makaazi yake kuanzia saa 10 Alfajiri, kwa lengo la kumzuia kufika Mahakamani kusikiliza kesi inamyomkabili Lissu.