
Mahakama nchini Tanzania imemfunguliwa mashtaka ya uhaini kiongozi wa chama cha upinzani Tundu Lissu kutokana na matamshi yake aliyotoa wiki iliyopita akiwataka wananchi kuzuia uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Lissu, mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA ambaye pia alimaliza katika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa rais wa 2020, alikamatwa Jumatano baada ya mkutano wa hadhara katika mkoa wa kusini magharibi mwa Ruvuma.
Baada ya kufikishwa mahakamani katika Mji Mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam, Lissu hakuruhusiwa kujibu mashtaka hayo ya uhaini.
Aidha alikanusha shtaka lengine tofauti la kuchapisha habari za uongo.
Mashtaka dhidi ya Lissu yameibua mjadala kuhusu suala la haki za binadamu kwenye taifa hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa urais ambao rais Samia Suluhu Hassan anawania tena.
Alipoingia madarakani Hassan mwaka wa 2021 kulikuwa na matumaini ya kumalizika kwa kile kilitajwa kama ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa na udhibiti wa vyombo vya habari uliofanyika chini ya utawala wa mtangulizi wake, John Magufuli.
Licha ya matumaini ya raia wa Tanzania kwa utawala wa rais Samia, amekosolewa pakubwa na wanaharakati wa haki za binadamu kutokana na msururu wa kukamatwa na kutekwa nyara bila maelezo na mauaji ya wapinzani wa kisiasa.
Hassan amesema serikali imejitolea kuheshimu haki za binadamu na aliagiza uchunguzi ufanyike kuhusu matukio ya utekaji nyara yaliyoripotiwa mwaka jana.
Lissu amekuwa akiendeleza mikutano kwenye maeneo mbalimabli ya nchi chini ya kauli mbiu “ No reforms, no election” kwa maana ya bila ya mageuzi hakuna uchaguzi.