Tanzania: Chama cha upinzani cha CHADEMA kimeondolewa kwenye uchaguzi wa 2025

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimeondolewa kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, afisa mkuu wa tume ya uchaguzi amesema siku ya Jumamosi, siku chache baada ya kiongozi wa chama hicho kushtakiwa kwa uhaini kwa madai ya kutaka kuvuruga uchaguzi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amesema CHADEMA imeshindwa kutia saini waraka wa maadili uliotarajiwa Jumamosi na hivyo kubatilisha ushiriki wake katika uchaguzi wa urais na wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mosi.

“Chama chochote ambacho hakikutia saini kanuni za maadili hakitashiriki uchaguzi mkuu,” mesema na kuongeza kuwa marufuku hiyo pia itahusu chaguzi zote ndogo hadi mwaka 2030.

Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, aliyekuwa mgombea urais, alifunguliwa mashtaka ya uhaini siku ya Alhamisi.

Uamuzi wa kukiondoa chama chake utaongeza uchunguzi wa rekodi ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu haki za binadamu anapowania kuchaguliwa tena.

Wanaharakati wa haki na vyama vya upinzani wameishutumu serikali ya Samia Suluhu Hassan kwa kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa, wakitaja msururu wa utekaji nyara na mauaji yasiyoelezeka.

Serikali imekanusha madai hayo na imefungua uchunguzi kuhusu utekaji nyara unaoripotiwa.

Chama cha Samia Suluhu Hassan Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilisema siku za nyuma kuwa serikali inaheshimu haki za binadamu na ilikanusha kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu.

CHADEMA haikuzungumza mara moja kuhusu uamuzi wa tume ya uchaguzi.

Mapema Jumamosi, chama hicho kilisema hakitashiriki katika hafla ya utiaji saini wa kanuni za maadili ya uchaguzi, kama sehemu ya msukumo unaofanya kufanya mageuzi.

Waendesha mashtaka walimtuhumu Lissu siku ya Alhamisi kwa kutoa wito kwa umma kuanzisha uasi na kuzuia uchaguzi usifanyike.

Hakuruhusiwa kujibu shtaka la uhaini, ambalo lina adhabu ya kifo.

Hapo awali CHADEMA ilitishia kususia uchaguzi labda mageuzi makubwa yafanyike kwenye mchakato wa uchaguzi ambao inasema ni kwa manufaa ya chama tawala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *