Tamasha la teknolojia za fedha lilioanza jana Juni 13, 2025 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam limatajwa kuwa miongoni mwa matamasha bora zaidi ya teknolojia duniani.
Tamasha hilo linalohusiaha wataalamu kutoka nchini 17 duniani linatarajiwa kuwanufaisha wataalamu wa Tanzania na taifa kwa ujumla huku ubunifu wa teknolojia ukitajwa kuwa chachu ya kukuza uchumi vijijini.
Akizungumzia tamasha hilo, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Estern Star Counsulting Group ambao pia huandaa tuzo za Top 100 Companies amesema tamasha hilo linatoa fursa ya mbalimbali zinazosaidia kukuza teknolojia ya kifedha pamoja na kuinua uchumi kwa njia ya teknolojia.
Imeandaliwa na @moseskwindi