Taliban: Iran ni mfano wa kwanza wenye mafanikio wa kuunda utawala wa Kiislamu katika zama hizi

Mkuu wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Muda ya Afghanistan inayoongozwa na Taliban amesema kuasisiwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfano wa kwanza wenye mafanikio wa kuunda utawala wa Kiislamu katika zama za sasa na kwamba utawala huo umekuwa na taathira kwa matukio ya kikanda.