Takwimu 5 kali ndani ya rekodi NBA

ARIZONA, MAREKANI: MSIMU mrefu wa NBA 2024-25 unaelekea ukingoni ukiwa umejaa rekodi mpya na matukio ya kukumbukwa. Zikiwa zimesalia saa chache tu kabla ya msimu wa kawaida kufungwa, haya hapa ni mambo matano yaliyovutia macho ya wengi.

1. THUNDER WAMEUPIGA MWINGI

Oklahoma City Thunder imeandika historia kwa kuwa timu yenye tofauti kubwa zaidi ya pointi katika msimu mmoja wakizidi wapinzani wao kwa wastani wa pointi +12.6 kwa mchezo, tofauti bora zaidi katika historia ya misimu 79 ya NBA.

  • Rekodi ya tofauti ya pointi bora zaidi:

Timu                Msimu      W-L        PCT        Tofauti ya Pointi

Oklahoma    2024-25     66-14      825             +12.6

L.A. Lakers   1971-72      69-13     841             +12.3

Milwaukee    1970-71      66-16     805             +12.3

Chicago         1995-96      72-10     878             +12.2

Thunder pia wamevunja rekodi kwa kushinda michezo 38 kwa tofauti ya pointi 15 au zaidi, zaidi ya rekodi ya awali (37) ya Bucks mwaka 1970-71.

Na zaidi wanatoa ‘turnovers’ yani kupindua matokeo 5.3 chache kwa mchezo kuliko wapinzani tofauti bora zaidi katika miaka 37.

Katika mechi 28 walizopitwa kwa pointi 10 au zaidi, wameshinda 18 asilimia ya mafanikio ya 64.3%, rekodi bora kabisa tangu takwimu hizi zianze kurekodiwa.

Rekodi yao dhidi ya timu za Mashariki? 29-1 bora zaidi katika historia dhidi ya mkondo tofauti.

2. WAZEE WA MIPANGO  (Offense & Defense)

Kwa msimu wa tatu mfululizo, Boston Celtics wanakaribia kuwa timu pekee katika historia ya NBA yenye nafasi ya juu 5 kwenye ufanisi wa kushambulia na wa kujilinda.

Tangu mwaka 1977-78 (ulipoanza kurekodiwa turnovers), hakuna timu iliyowahi kuingia top 5 kwa pande zote mbili kwa misimu mitatu mfululizo mpaka sasa.

Timu    Msimu 1       Nafasi    Msimu 2       Nafasi   Ubingwa

Boston  2022-23         2, 2     2023-24           1, 2         1

Boston  2024-25 (c)   1, 5         N/A        N/A        ?

Hii inaashiria uimara mkubwa wa mfumo wao si tu timu yenye vipaji, bali yenye uthabiti na uwiano mzuri.

3. REKODI YA MASHUTI

Boston Celtics wanaongoza katika asilimia ya mashambulizi yao kutoka nje ya mstari wa pointi tatu: 53.6% ya mashuti yao yote ni ya 3-point kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa.

Kwa jumla ya ligi, msimu huu:

  • 42.1% ya mashuti yote ni ya 3-point (rekodi ya juu zaidi kuwahi kutokea)
  • Wastani wa mashuti ya mid-range umeporomoka hadi chini ya 10% kwa mara ya kwanza
  • Mashuti ndani ya paint yameendelea kuwa asilimia kubwa (zaidi ya 57% kwa misimu mitatu mfululizo)

Msimu %     Paint %      Mid-range      % 3-point

2020-21         56.1%         12.9%              39.2%

2024-25         57.1%            9.8%              42.1%

Hii ni ishara ya mabadiliko makubwa katika NBA, ambapo hesabu zinaelekeza mashambulizi zaidi kwenye maeneo ya faida kubwa paint na 3-point.

4.  UBORA WA AJABU

Cleveland Cavaliers wameonyesha ukali wa kupiga mashuti wakiwa timu pekee iliyo ndani ya top 5 kwa asilimia ya mashuti ya 3-point na mafanikio katika mashuti hayo.

  • 3PT Rate: 45.8% (nafasi ya 4)
  • 3PT Accuracy: 38.4% (nafasi ya 1)
  • Effective FG%: 58.1% – kiwango bora zaidi katika historia ya NBA

Wao pia ndio timu pekee yenye wachezaji watatu walio na eFG% ya zaidi ya 60% kati ya wachezaji wote waliojaribu mashuti 500+:

  • Jarrett Allen – 71.1% (nafasi ya 1)
  • Evan Mobley – 60.7%
  • Ty Jerome – 60.4%

Kwa takwimu hizi, Cavs wanabeba moja ya safu bora kabisa za kushambulia katika historia ya NBA.

5. NGOME YA CHUMA

Katika ulinzi, Dyson Daniels wa Atlanta Hawks ameweka historia kwa wastani wa 3.0 steals kwa mchezo, akimzidi mchezaji wa pili kwa 1.2 steals angekuwa wa kwanza kwa wastani huo tangu 1993-94.

Zaidi ya hayo. Daniels ana wastani wa 5.8 deflections kwa mchezo  wa juu zaidi tangu “hustle stats” zilipoanza kurekodiwa.

Kwa upande mwingine, licha ya kuumia kabla ya All-Star break, Victor Wembanyama amebaki kuwa mchezaji mwenye blocks nyingi zaidi 3.8 kwa mchezo, kiwango bora zaidi katika miaka 26.

Pia ana wastani wa blocks kwa foul: 1.68  rekodi bora zaidi katika historia ya NBA.

Mchezaji                            Msimu  Blocks    Fouls      Ratio

Victor Wembanyama     2024-25   176         105         1.68

Victor Wembanyama     2023-24    254         153         1.66

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *