Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TET) imewapa tuzo walimu wa shule za msingi na sekondari waliofanya vizuri katika stadi za ufundis…

Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TET) imewapa tuzo walimu wa shule za msingi na sekondari waliofanya vizuri katika stadi za ufundis…

Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TET) imewapa tuzo walimu wa shule za msingi na sekondari waliofanya vizuri katika stadi za ufundishaji nchini ikiwa ni mara ya tatu kwa walimu wa msingi na mara ya kwanza kwa walimu wa sekondari.

Tuzo hizo zimetolewa leo Juni 14, 2025 katika ukumbi wa Maktaba uliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akitoa neno la utangulizi, Mkurugenzi wa TET, Dkt. Aneth Komba amesema shindano hilo limehusisha walimu wa masomo ya hisabati na masomo ya sayansi ya fizikia, kemia na baiolojia kwa kidato cha kwanza likiwalenga walimu katika ngazi ya halmashauri, kanda na taifa.

Kwa mwaka huu TET ilikusanya video 10 kutoka halmashauri 184 na kupata jumla ya video 1,840 zilizoshindanishwa.

Miongoni mwa vigezo vilivyotumika katika kupata washindi ni pamoja na matumizi yanayopigiwa chapuo na serikali ya TEHAMA katika ufundishaji.

Shindano la ubunifu katika ufundishaji na ujifunzaji ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu.

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *