
Taarifa za chuki zimeongezeka kwenye mitandao ya Meta, ikiwemo Facebook na Instagram, tangu kampuni hiyo kukatisha mkataba na kukagua taarifa za kweli kwenye mitandao, iliokuwa ikiendeshwa na kampuni ya Palo Alto, utafiti wa hivi punde umebaini.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kusitisha kwa ukaguzi wa taarifa kwenye mitandao hiyo, kulifanyika mwezi Junuari wengi wakitazama hatua hiyo kuwa mpango wa utawala wa Rais Donald Trump, kuruhusu uhuru wa kujieleza.
Kampuni hiyo ya Meta pia iliondoa marufuku ya uchapishaji taarifa za dhuluma za kijinsia, hatua ambayo iliruhus watu kuanza kuchapisha vídeo na taarifa kuhusu maswala ya vitendo vya ndoa.
Zaidi ya watu alfu 7,000 waliohojiwa wamesema kwa sasa hawako huru kutumia mitandao ya kijamii, kutokana na taarifa nyingi ya kupotosha na ukosefu wa usalama mitandao.
Licha ya utafiti huu Kampuni ya Meta imesisitiza kwamba mabadiliko hayo mitandao yake ni salama kwa watumiaji.