Syria: Israeli yafanya mashambulizi yake makali zaidi ili ‘kulinda’ jamii ya Druze

Zaidi ya mashambulio 20 ya Israeli yamelenga maeneo ya kijeshi kote Syria usiku wa Ijuma Mei 2 kuamkia Jumamosi Mei 3, mashambulizi ya “makubwa zaidi” mwaka huu, shirika lisilo la kiserikali limesema, baada ya Israeli kutangaza shambulio karibu na ikulu ya rais huko Damascus.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 4

Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la serikali ya Syria SANA limetangaza kuwa “raia mmoja ameuawa,” huku jeshi la Israeli likithibitisha kuwa limelenga miundo mbinu ya kijeshi karibu na mji mkuu wa Syria, nchi ambayo Israeli bado iko vitani dhidi yake. “Zaidi ya mashambulizi 20 ya Israeli yamelenga maghala na maeneo ya kijeshi huko Deraa, karibu na Damascus na katika maeneo ya Hama na Latakia,” Shirika la la Haki za Kibinadamu la Syria (SOHR) lilitangaza mapema, ambalo lina mtandao mkubwa wa vyanzo katika nchi hiyo yenye vita. Shirika hilo lisilo la kiserikali limebaini kwamba mashambulizi hayo “yalikuwa makubwa zaidi tangu mwanzoni mwa mwaka.”

Waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP katika mji mkuu wamesikia sauti ya ndege na milipuko kadhaa. Shirika la habari la Syria SANA, ambalo lilikuwa limeripoti matukio kadhaa karibu na Damascus na kote nchini, limesema kuwa “raia mmoja aliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israeli pemezoni mwa Harasta, karibu na Damascus.”

Tangu kuangushwa kwa rais Bashar Al Assad mwezi Desemba, Israeli ambayo inatilia shaka mamlaka mpya, imefanya mamia ya mashambulizi kwenye maeneo ya kijeshi nchini Syria, ikisema inataka kuzuia silaha zisianguke mikononi mwa mamlaka mpya, ambayo inaitaja kuwa ya “wanajihadi.” Israel pia imetuma wanajeshi katika eneo lisilo na wanajeshi katika eneo lenye milima la Golan.

“Kuongezeka kwa uhasama hatari”

Mnamo Mei 2, alfajiri, Israeli ilitangaza kuwa ilifanya mashambulizi karibu na ikulu ya rais Ahmed Al-sharaa, kama onyo dhidi ya shambulio lolote dhidi ya jamii ya walio wachache ya Druze nchini Syria. Kile ambacho rais wa Syria alikiita “kuongezeka kwa uhasama hatari” pia kimelaaniwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Mashambulizi ya Israeli yamekuja baada ya ghasia za kidini mapema wiki hii kati ya makundi yenye silaha yanayohusishwa na serikali ya Syria na wapiganaji wa Druze ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 100 karibu na Damascus na kusini mwa nchi jirani ya Israeli, kulingana na shirika la Haki za Binadamu nchini Syria. “Huu ni ujumbe wa wazi uliotumwa kwa utawala wa Syria. “Hatutaruhusu vikosi vya (Syria) kutumwa kusini mwa Damascus au kutishia jamii ya Druze kwa njia yoyote,” Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa Ulinzi, Israel Katz, wamesema.

Lakini usaidizi huu wa vurugu hutumika hasa kwa maslahi ya Israeli, anaelezea mkazi wa Druze wa Jaramana, aliyewasiliana na Alice Froussard wa RFI na ambaye alipendelea kutotajwa jina. “Israel inajaribu sana kugawanya watu ili kugawanya ardhi, kwa sababu ni lengo lao pia kuchukua miji kama Sweida, Daraa na maeneo ya kusini mwa Syria. Waisraeli wanataka kuchukua ardhi yetu, wanataka kuteka sehemu za Syria. Wanatumia vurugu hizi za kidini kama kichocheo, wanazitumia kama ulivyofanya utawala wa Bashar Al Assad kabla yao.”

Jeshi la Israeli limewekwa kwa idadi kubwa huko Syria kwenye Jabal al Sheikh, kwa jina lingine la Mlima Hermoni. Linazuia ufikiaji wa Milima ya Golan na limepata mafanikio tangu kuanguka kwa Bashar Al Assad. Wakati huo huo, kwa mujibu wa mtafiti wa Syria Charles Lister, Israeli haitaki dola yenye nguvu upande wake, na hata “inataka kuhimiza mabadiliko ya utawala.” Kuhusu waziri wa fedha wa mrengo mkali wa kulia wa Israeli, Bezalel Smotrich, alitangaza mapema wiki hii: “Israel lazima isambaratishe Syria.”

Nchi kadhaa zapaza sauti na kutaka vita vikome

Qatar ilishutumu kama “uchokozi wa wazi dhidi ya uhuru” wa Syria na Saudi Arabia “ilithibitisha kukataa kwa uchokozi wa Israel na kudhoofisha uthabiti” wa Syria. “Syria lazima isiwe uwanja wa michezo wa mivutano ya kikanda,” imeonya Ujerumani, ikitoa wito kwa serikali mpya ya Syria kuhakikisha “ulinzi wa raia” na “wahusika wote” kutekeleza “vizuizi kubwa zaidi.”

Israeli ilikuwa imetishia kuchukua hatua “kwa nguvu” ikiwa Damascus haitalinda jamii yake ya Druze. Tangu muungano unaoongozwa na Waislam wa madhehebu ya Sunni uingie madarakani tarehe 8 Desemba, Israeli imedai kutetea haki ya jamii ya walio wachache ya Druze nchini Syria. Jamii hii ya wasomi, ambayo inatoka katika tawi la Uislamu wa madhehebu ya Washia, pia imeanzishwa nchini Israeli na Lebanoni.

Katika muktadha huu, Ahmed Al-sharaa Shareh alipokea Mei 2 huko Damascus kiongozi wa Druze kutoka Lebanon Walid Joumblatt, ambaye alikuwa amewaita wafuasi wake wa kidini nchini Syria “kukataa kuingiliwa na Israeli.” Siku ya Ijumaa, Mei 2, OSDH pia iliripoti kwamba wapiganaji wanne wa Druze waliuawa wakati wa mchana katika shambulio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *