
Nchini Sudan, ghasia zimefikia kiwango kipya wikendi hii kuanzia Aprili 11 hadi Aprili 13 huko Darfur. Kwa mujibu wa vyanzo vya kibinadamu vya ndani, zaidi ya raia mia moja wameuawa tangu siku ya Ijumaa, Aprili 11, katika mfululizo wa mashambulizi yanayohusishwa na vikosi vya kijeshi vya Jenerali Hemetti, ambavyo vimekuwa vikijaribu kuunganisha nguvu zao huko Darfur tangu kupoteza mji wa Khartoum unaoshikiliwa na jeshi la Sudani.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wanamgambo wa RSF walifanya mashambulizi katika ambi ya watu waliohamishwa ya Zamzam nje kidogo ya El Fasher, mji wa mwisho huko Darfur ambao hauko chini ya udhibiti wa wanamgambo.
Mnamo Aprili 13, msemaji wa RSF nchini Sudan alihakikisha kwamba sasa wamechukua udhibiti wa kambi ya Zamzam, ambayo inahifadhi wakimbizi wa ndani wasiopungua 500,000, ambao wanakabiliwa na njaa, kulingana na Umoja wa Mataifa. Hakuna chanzo huru ambacho kimeweza kuthibitisha hili.
Kambi ya Zamzam imekuwa eneo la mashambulizi ya mara kwa mara tangu kuanza kwa vita hivi, lakini tangu Aprili 11, ghasia zimeongezeka. Kulingana na vyanzo vya misaada ya kibinadamu, wanamgambo hao kwanza walishambulia eneo hilo kwa saa kadhaa kabla ya kuvuka eneo la kambi hiyo kwa njia ya ardhini na kushambulia.
Wafanyakazi wa misaada wauawa
Miongoni mwa raia waliouawa ni wafanyakazi tisa wa misaada, wafanyakazi wa hospitali ya mwisho iliyokuwa ikifanya kazi katika eneo hilo. “Walipigwa risasi na kufa,” anashtumu afisa kutoka Relief International,shirika lisilo kuwa la kiserikali lililowaajiri. Kulingana na chanzo hiki, mamia ya makazi ya muda na soko kuu la kambi hiyo pia viliharibiwa, wakati kambi ya Zamzam tayari imetangazwa kuwa eneo lenye njaa kutokana na kizuizi kilichowekwa na FSR, ambayo inauzingira mji wa El Fasher.