
Nchini Sudani Kusini, hali ya wasiwasi inaongezeka tena licha ya wito wa kuheshimiwa kwa makubaliano ya amani. Chini ya mkataba huu uliotiwa saini mwaka wa 2018, serikali ya umoja wa kitaifa na mpito iko mjini Juba.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux
Rais Salva Kiir na mpinzani wake wa kihistoria, Makamu wa Rais Riek Machar, kwa hivyo wanagawana madaraka. Lakini tangu mwanzoni mwa mwaka, makabiliano ya moja kwa moja kati ya vikosi vyao vya kijeshi yameripotiwa katika mikoa kadhaa. Na jana, Jumanne Februari 25, upinzani ulishutumu kulipuliwa kwa kambi yake moja ya kijeshi na jeshi la Sudani Kusini kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Mapema asubuhi, picha za helikopta ya kijeshi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikibainisha “mashambulizi ya mabomu” katika Kaunti ya Ulang huko Upper Nile. Msemaji wa jeshi la upinzani la Riek Machar kisha alishutumu kwenye Facebook, kisha kwenye vyombo vya habari vya ndani, “ukiukaji” uliofanywa na jeshi la Sudani Kusini. “Vituo vya mkutano” vya vikosi vya upinzani vilisahmabuliwa kwa mabomu na jeshi la serikali, kulingana na msemaji wao.
Katika taarifa, msemaji wa jeshi la Sudani Kusini hakuthibitisha shambulio hilo, lakini alizungumza juu ya operesheni ya “ukaguzi”. Kulingana na msemaji wa jeshi la Sudani Kusini, “kwa wiki mbili” jeshi la upinzani na White Army, wanamgambo wa mchungaji kutoka jamii ya Nuer, “wamehamasisha idadi kubwa ya vikosi.” Wanasemekana kupanga kuzuia kutumwa kwa jeshi la Sudani Kusini huko Nasir na kushambulia kaunti ya Baliet, kulingana na msemaji wa jeshi. Mapigano makali yalizuka huko Nasir mnamo Februari 14 na 15, yakihusisha jeshi la Sudani Kusini na vijana kutoka jamii ya Nuer waliojihami kwa silaha.
Umoja wa Mataifa unasema “una wasiwasi mkubwa na ripoti za kuongezeka kwa machafuko huko Upper Nile” na kutoa wito wa utulivu.