Sudani Kusini: Upinzani wavunja makubaliano ya amani baada ya kukamatwa kwa Riek Machar

Nchini Sudan Kusini, ongezeko la vita vya wenyewe kwa wenyewe linaendelea. Jioni ya Machi 26, Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar amewekwa chini ya kizuizi cha nyumbani na vikosi vya usalama vya Sudani Kusini.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kukamatwa huko kunakuja baada ya wiki kadhaa za mvutano, uliosababishwa na kukamatwa kwa baadhi ya wafuasi wake na mapigano karibu na mji wa Nasir mnamo Machi 4, ambapo afisa wa cheo cha jenerali katika jeshi la serikali aliuawa na kundi lenye silaha linaloaminika kuwa na uhusiano wa karibu na Riek Machar.

Jumuiya za kikanda na Umoja wa Mataifa, unahofia kurejea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini.

Kukamatwa kwa Machar, kumezua wasiwasi wa nchi hiyo kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Jumuiya ya nchi za IGAD imetoa wito kwa pande zote kutanguliza mazungumzo kutatua changamoto zilizopo.

Umoja wa Mataifa, umeonya kuwa, kuvunjika kwa mkataba wa amani wa mwaka 2018 kunatishia kurejea kwa vita nchini Sudan Kusini na maisha ya wananchi wa taifa hilo yako hatarini.

Kwa wiki kadhaa sasa, Sudan Kusini imekuwa kwenye hatari ya kurejea kwa vita kufuatia serikali ya rais Salva Kiir kuwatuhumu waasi wa White Army, wanaoripotiwa kuungwa mkono na Machar kuvamia kambi ya jeshi katika jimbo la Upper Nile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *