Sudani Kusini: UNSC yaongeza muda wa UNMISS kwa mwaka mmoja

Baada ya majuma kadhaa ya mazungumzo makali, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kikosi cha kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa mwaka mmoja, huku likitaka kusitishwa mara moja kwa mapigano kati ya pande hasimu. Ujumbe huo, ambao unaweza kujumuisha hadi wanajeshi 17,000 na maafisa wa polisi 2,100, unaweza kurekebisha idadi na kazi zake kulingana na hali ya usalama nchini. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Idadi kubwa ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, likiongozwa na Marekani, hawajaridhishwa na jinsi serikali ya mpito inavyoshughulikia UNMISS nchini Sudani Kusini na wanahofia kwamba kikosi cha Umoja wa Mataifa hakitaweza kutekeleza jukumu lake la kuleta utulivu. Hatari ya Sudani Kusini kurejea kwenye mzozo wa kikabila bado iko juu kutokana na kuanza kwa mapigano, amesema Kaimu Balozi wa Marekani Dorothy Shea. Baadhi ya wajumbe wa Baraza pia wameitaka serikali ya mpito kuacha kuzuia kazi ya UNMISS kwa kuweka vikwazo vya usafiri.

“Ili kufikia amani na kuepusha kuzuka tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, serikali ya mpito kwa hiyo lazima ichukue hatua haraka. Ili kumaliza ghasia na kutuliza mivutano ya kisiasa, Makamu wa Rais Machar lazima aachiliwe kutoka kizuizini na suluhu lazima ifikiwe kati ya pande zinazohusika.

Hata hivyo, Washington inakataa kutenga fedha zaidi kwa ajili ya uchaguzi “unaocheleweshwa mara kwa mara”. Urusi, China na Pakistan zilijizuia kupiga kura kuhusu kuongezwa muda kwa UNMISS, ili “kutetea uhuru” wa nchi hiyo changa. Kundi la Baraza la Kiafrika, ambalo lilipiga kura ya kuunga mkono, hata hivyo limeangazia ombi la Sudani Kusini la kusasishwa mara kwa mara kuhusu uhamisho wa kituo cha Topping. Uhamisho ambao UNMISS na serikali ya mpito inasemekana kukubaliana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *