
Tume iliyopewa jukumu la kusimamia utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya mwaka 2018 nchini Sudani Kusini imetaka kuzingatiwa kwa masharti yake ikiwa ni pamoja na kuachiliwa huru kwa Makamu wa Rais wa Sudani Kusini Riek Machar ambaye amekuwa akizuiliwa na rais. Wakati tume hii iliyoundwa na kambi ya kikanda ya Afrika Mashariki IGAD inatoa angalizo la kutisha, inakumbusha kuwa makubaliano haya yanasalia kuwa “msingi” wa utulivu wa baadaye wa nchi.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux
Nchini Sudani Kusini, wito mpya ulitolewa Aprili 28, 2025, wa kuachiliwa kwa Makamu wa Rais Riek Machar na wanachama wengine wa upinzani wanaozuiliwa na kwa agizo la rais Salva Kiir tangu mwezi uliopita. Wito huo unatokana na tume inayosimamia utekelezaji wa makubaliano ya amani, tume iliyoundwa na jumuiya ya kikanda ya Afrika Mashariki, Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD).
Ikiwa ni aina ya msuluhishi wa mchakato wa amani, tume ilitoa ripoti yake ya robo mwaka siku ya Jumatatu, ambayo inajumuisha miezi ya Januari, Februari na Machi 2025, kipindi ambacho hali ilizorota sana nchini Sudani Kusini.
“Bado kuna nafasi ya mazungumzo”
“Matukio ambayo hayajawahi kushuhudiwa tangu kutiwa saini kwa makubaliano miaka sita iliyopita”: hivi ndivyo tume inayosimamia mchakato wa amani inavyoelezea matukio ya wiki za hivi karibuni. Wakati pande zote mbili zikilaumiwa kwa ukiukaji wa usitishaji mapigano, ni kambi ya Salva Kiir ambayo imetengwa kwa kile kinachoitwa ukiukaji wa “kisiasa”: kuzuiliwa kwa Riek Machar, mwaliko wa jeshi la Uganda bila kushauriana na watia saini wengine, na mabadiliko ya baraza la mawaziri yanachukuliwa kuwa “ya upande mmoja.”
Mapigano yanaendelea kati ya upinzani na vikosi vya serikali, lakini waangalizi wa makubaliano ya amani wanataka kuamini kwamba yote hayajapotea. “Ingawa uaminifu kati ya wahusika umetikiswa sana,” wanaandika, “bado kuna nafasi ya kushirikishwa tena na mazungumzo.”
Kwa hiyo wanadai kuachiliwa “mara moja” kwa Riek Machar na maafisa wengine wote wa upinzani wanaozuiliwa, “isipokuwa ushahidi wa kuaminika unahalalisha kesi za kisheria.” Hatimaye, wanatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama “katika pande zote” na kutambua kwa wasiwasi kusitishwa kwa maandalizi ya uchaguzi, ambao unatarajiwa kufanyika “chini ya miezi 20.”