
Nchini Sudani Kusini, mvutano kati ya wanajeshi wa Rais Salva Kiir na wale wa Makamu wa Rais Riek Machar umekuwa ukiongezeka tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika jimbo la Equatoria Magharibi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux
Wakati pande zote mbili zikirejelea kujitolea kwao kutekeleza makubaliano ya amani, hadithi zao za matukio ya hivi majuzi ya usalama zinatofautiana kwa kiasi kikubwa. Huko Equatoria Magharibi, jeshi la Sudan Kusini linalomtii Rais Salva Kiir limedai kukumbana na uhasama kutoka kwa wanajeshi wa upinzani, watiifu kwa Riek Machar, wakati wa kuvunjwa kwa vituo vya ukaguzi, uvunjaji ulioamuliwa wakati wa Jukwaa la Magavana mwishoni mwa mwaka 2024.
Lakini jeshi la Riek Machar limeshutumu shambulio hilo na kutekwa kwa moja ya kambi zake na jeshi la Sudani Kusini. Tukio ambalo, ikiwa litathibitishwa na vyombo vinavyofuatilia makubaliano ya amani, halitakuwa la kawaida, ikizingatiwa kwamba usitishaji wa mapigano umekuwepo tangu mwaka 2018.
Akiwasiliana na RFI, Kanali Lam Paul Gabriel, msemaji wa jeshi la upinzani, hata hivyo anasisitiza kuwa Equatoria Maharibi iko shwari. Lakini anabaini kwamba jeshi la Sudani Kusini “limevuka mstari” na haliondoi uwezekano wa mashambulizi zaidi. “Mazungumzo mengi” kwa sasa yanafanyika ili kukomesha ghasia, amesema.
Huko Upper Nile, kaskazini-mashariki mwa nchi, hali ya wasiwasi imesalia kuwa kwenye kiwango cha juu huko Nasir, ambapo mapigano makali yaliripotiwa tarehe 14 na 15 Februari kati ya jeshi la Sudani Kusini na raia vijana wenye silaha, mara nyingi waliwasilishwa kama wanachama wa Jeshi la White, wanamgambo wa kikabila ambao kwa kiasi kikubwa watiifu kwa upinzani. Kutokana na ongezeko wa uhasama huo, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia yanataka makubaliano ya amani yaheshimiwe.