
Mapigano yamezuka katika mji wa Nasir, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, siku ya Jumatatu Machi 3 kati ya jeshi la Sudani Kusini na wapiganaji wa kund la White Army, wanamgambo wa jamii walio karibu na makamu wa rais na mpinzani Riek Machar. Mapigano haya yanatokea licha ya juhudi za Riek Machar kujaribu kupunguza hali ya wasiwasi mwishoni mwa juma.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux
Mapigano yalizuka huko Nasir katikati ya mwezi wa Februari na jeshi la Sudan Kusini lilituma wanajeshi kutoka Malakal kubadilihana na wanajeshi walioko Nasir, ambapo hakukuwa na uhusiano mzuri na wakazi wa eneo hilo. Kutumwa kwa wanajeshi hao kulichukuliwa kuwa tishio.
Siku ya Jumamosi, Machi 1, Makamu wa Rais Riek Machar alitangaza kuundwa kwa kamati mbili zinazojumuisha viongozi wa kimila kutoka kaunti za Ulang na Nasir. Jukumu lao ni kuandamana na majahazi ya jeshi la Sudani Kusini yaliyotumwa kutoka Malakal kwenye Mto Sobat hadi Nasir. Na kuzuia shambulio lolote la vijana kutoka kundi la wanamgambo wa White Army.
Hali ya utulivu ya hali ya juu ilitawala mjini Nasir siku ya Jumapili, na baadae kijana mmoja wa kutoka kundi la wanamgambo la White Army aliuawa alasiri na jeshi la Sudani Kusini, kulingana na Ter Manyang Gatwech, kutoka shirika la kiraia la Center for Peace and Advocacy (CPA). Mapigano makali yalizuka mwendo wa saa 10 alfajiri siku ya Jumatatu na mashambulizi ya anga yaliripotiwa.
Mkutano wa ofisi ya rais ulifanyika Juba
Kutokana na mlipuko huu mpya wa ghasia huko Upper Nile, mkutano wa ofisi ya rais ulifanyika Juba siku ya Jumatatu. Kwa mujibu wa mwanaharakati wa mashirika ya kiraia Edmund Yakani, aliyehudhuria mkutano huo, Rais Salva Kiir, Makamu wa Rais Riek Machar na makamu wengine wanne walikariri kwamba vikosi vilivyotumwa Nasir havikuwa na nia ya kuwapokonya silaha wapiganaji wa kundi la wanamgambo la White Army. Waliomba kwenye ukurasa wa Facebook wa ofisi ya rais, “wakazi kuruhusu kupita kwa usalama kwa wanajeshi hadi wafike kambi zao huko Nasir. “