
Wiki moja baada ya Makamu wa Rais Riek Machar kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani na vikosi vya usalama vya Rais Salva Kiir, mipango ya upatanishi inaanza kutekelezwa.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux
Kufuatia ziara ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kama mjumbe maalum, ujumbe wa ngazi ya juu ukiongozwa na Domitien Ndayizeye, rais wa zamani wa Burundi, na Effie Owuor, jaji mstaafu wa Kenya, ambao wote ni wajumbe wa Jopo la Wazee wa Busara la Umoja wa Afrika (Panel of Wise), wataanza safari ya siku tano huko Juba.
Je, upatanishi wa Umoja wa Afrika, unaowasili Sudani Kusini leo Jumatano, Aprili 2, utafanikiwa kuvunja mkwamo wa kisiasa uliopo Juba? Haya ndiyo matumaini ya Joram Biswaro, balozi wa Umoja wa Afrika nchini Sudani Kusini. Alihojiwa na RFI, alisema kuwa ziara ya Jopo la Watu Wenye Hekima ni “misheni ya mshikamano na watu wa Sudani Kusini kuona jinsi mgogoro unaweza kutatuliwa.”
Ameongeza kuwa wakati mvutano bado uko kwenye kilele na hofu ya kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe haijawahi kuwa kubwa zaidi: “Mazungumzo ndiyo njia pekee ya kupata suluhu.”
Vyovyote iwavyo, kazi ya ujumbe wa Umoja wa Afrika, ambao unatakiwa kubaki nchini humo kwa siku tano, inazidi kuwa ngumu. Siku ya Ijumaa, Machi 28, Raila Odinga hahukuruhusiwa kukutana na Riek Machar.
Kikwazo ambacho kikundi cha wapatanishi kinatarajia kushinda. Balozi Joram Biswaro anaeleza kwamba nia ya Jopo la Wenye Hekima ni kweli “kuzungumza na kila mtu: rais, makamu wa kwanza wa rais, makamu wa rais wengine na vyama vya kisiasa, pamoja na makanisa na mashirika ya kiraia (…) ili Sudani Kusini itoke kwenye mgogoro huu.”
Jopo la Wazee wa Busara lililoanzishwa mwaka 2007, linalenga kuunga mkono juhudi za Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, hasa katika sekta ya kuzuia migogoro. Jopo hili pia lilitoa wito siku ya Jumatatu “kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa Makamu wa Rais Riek Machar.”
Kama ukumbusho, imepita wiki moja tangu Makamu wa Rais Riek Machar kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani na vikosi vya usalama vya Rais Salva Kiir. Wito wa kuachiliwa kwake na kurejelewa kwa mazungumzo kati ya viongozi hao wawili ili kuokoa makubaliano ya amani ya 2018 umeongezeka.