
Jeshi la Sudani Kusini lilitekeleza mashambulizi ya anga usiku wa Jumapili, Machi 16, kwenye mji wa Nasir, huko Upper Nile (kaskazini mashariki mwa nchi). Mashambulizi haya yalisababisha vifo vya watu 21 kulingana na mamlaka ya eneo hilo, iliyonukuliwa katika vyombo vya habari vya Sudani Kusini.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux
Mji wa Nasir ambao unapatikana karibu na mpaka wa Ethiopia, umekumbwa na mapigano mabaya tangu katikati ya mwezi wa Februari 2025 kati ya jeshi la Sudani Kusini na wanamgambo wa Nuer, White Army, linalojulikana kuwa karibu na Makamu wa Rais Riek Machar. Afis wa cheo cha Jenerali katika jeshi la Sudani Kusini aliuawa wakati wa akiondolewa kwa helikopta ya Umoja wa Mataifa katika eneo la mapigano mnamo Machi 7, baada ya kambi ya kijeshi kutekwa na White Army.
Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Machi 17, msemaji wa serikali ya Sudani Kusini pia amethibitisha kuwepo kwa wanajeshi wa Uganda nchini Sudani Kusini. Awali alikanusha wakati jeshi la Uganda lilipotangaza Machi 11 uwepo wao nchini humo. “Vitengo vya ufundi na usaidizi”: Wakati hatimaye alithibitisha uwepo wa jeshi la Uganda nchini Sudani Kusini, Michael Makuei hakueleza kwa undani “Jeshi la Uganda,” alisema, “kwa sasa lipo Juba na Sudani Kusini, chini ya mkataba wa kijeshi kati ya serikali za Sudani Kusini na Uganda uliotiwa saini wakati wa Lord’s Resistance Army (LRA). Ni mkataba huu huu unaoendelea. “
“Mnatakiwa kukaa mbali.”
Kuanzia mwaka wa 2008, mkataba huu wa ushirikiano wa kijeshi umesasishwa ili kuhalalisha uwepo wa jeshi la Uganda katika eneo la Sudani Kusini. Misafara, ikiwa ni pamoja na mizinga, imerekodiwa ikivuka mpaka katika siku za hivi karibuni, kuelekea Juba. Hali inaonekana kuongezeka kwa mgogoro, na picha za wahasiriwa waliochomwa katika milipuko ya usiku huko Nasir hazivumiliki. Watumiaji wengi wa mtandao wameshutumu “uhalifu”. Lakini Michael Makuei anasema “hakuna raia aliyeathirika.” “Natoa wito kwa askari wote wa White Army wanaojiita raia kurejea nyumbani ambako wanachunga ng’ombe wao,” ameonya. Tunashauri Jeshi la White Army kuondoka katika mji wa Nasir sasa. (…) Jeshi letu la anga limefanya mashambulizi katika mji wa Nasir asubuhi ya leo. Watu wanaoishi katika mazingira magumu katika maeneo yenye uhasama, hilo ndilo tatizo lao. Mnatakiwa kukaa mbali na maeneo yenye uhasama ili mashambulizi ya anga yawalenge tu wapiganaji. Lakini ikiwa unajikuta katikati ya mapiano, hakuna tunachoweza kuokoa. “
Mashambulizi ya anga pia viliripotiwa na vyombo vya habari vya eneo hilo katika Kaunti ya Longochuk, ambayo inapakana na Kaunti ya Nasir, Jumapili usiku. Mtu mmoja aliuawa.