Sudani Kusini: Hospitali ya Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) yashambuliwa kwa bomu

Nchini Sudani Kusini, hospitali ya shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) katika mji wa kaskazini wa Old Fangak imeshambuliwa kwa bomu saa 10 alfajiri kwa saa za huko Jumamosi, Mei 3.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Duka la dawa na maghala yake yote ya dawa ameharibiwa, na kuwanyima zaidi ya watu 40,000 huduma muhimu, kulingana na shirika hilo, ambalo linalaani “ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu.” Vyombo vya habari vya Sudani Kusini vinaripoti kuwa shambulio hilo limesababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa. Jeshi la Sudani Kusini bado halijazungumzia tukio hilo.

Hatari ya kurudi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe

Hali ya usalama nchini Sudani Kusini imezorota katika miezi ya hivi karibuni, kutokana na mapigano kati ya vikosi vya Rais Salva Kiir na wale wanaomtii Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar, ambaye alikamatwa mwezi Machi.

Mivutano hii inazidisha hofu ya kurejea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka wa 2018 baada ya kusababisha vifo vya watu 400,000 katika nchi hii yenye wakazi milioni 11.

Kushambuliwa kwa hospitali ya MSF kunakuja siku moja baada ya mkuu wa jeshi Paul Majok Nang kutoa vitisho dhidi ya makundi hasimu katika kaunti za Fangak na Leer.

MSF imesema ndiyo hospitali pekee inayofanya kazi katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *