Sudani: Jeshi laendelea kusonga mbele mjini Khartoum na kuchukua udhibiti wa daraja la kimkakati

Mjini Khartoum, jeshi la Sudani, katika vita na wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) tangu Aprili 2023, linaendelea kusonga mbele hatu kwa hatua katika mji mkuu.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, Februari 25, 2025,vimechukuwa udhibiti wa daraja la kimkakati linaloelekea kituo cha utawala cha Khartoum na ambapo ikulu ya rais iko, ambayo iliangukia mikononi mwa RSF tangu kuanza kwa vita. Jeshi sasa linatarajia kukata usafirishaji wa silaha na chakula kwa RSF, ambayo imefanya eneo la katikati mwa jiji la Khartoum kambi yake kubwa zaidi ya kijeshi.

Baada ya siku kadhaa za mapigano makali, vyanzo vya kijeshi vimetangaza kwamba wamechukua udhibiti wa daraja la Souba, linaloelekea kusini mwa mji mkuu, sehemu ya mashariki na Bahri sasa iko mikononi mwa jeshi.

Video zilizorekodiwa na wanajeshi zinawaonyesha kwenye lango la daraja hili upande wa mashariki wa jiji. Daraja la Liberty, ambalo linaunganisha katikati mwa jiji kuelekea kusini, pia liko chini ya udhibiti wa jeshi, kulingana na chanzo kingine cha kijeshi. Madaraja kumi makuu yanaunganisha sehemu tatu za mji mkuu. Mengi ya madaraja haya sasa yanadhibitiwa na wanajeshi. Mapigano kwa sasa yanaripotiwa karibu na daraja la Jabal Awliya.

Jeshi linatafuta kudhibiti wanamgambo hao ili kuzuia usambazaji wa vifaa na chakula kwa RSF katikati mwa Khartoum. Vikosi vya Sudani vinasonga mbele polepole kuelekea Mtaa wa Sittin na soko kuu kusini mwa Khartoum.

Maendeleo pia yameonekana kusini mwa Omdurman ambapo ndege ya kijeshi ilianguka ikiwa na maafisa kadhaa, akiwemo Jenerali Bahr Ahmad Bahr. Ajali hiyo inakuja siku moja baada ya RSF kudai kuidungua ndege ya kivita huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini magharibi mwa nchi hiyo.