Sudani: Jeshi laendelea kusonga mbele katika mji mkuu wa Khartoum dhidi ya wanamgambo

Kufuatia kutekwa tena kwa ikulu ya rais mjini Khartoum, jeshi limeendelea kusonga mbele katika mji mkuu siku ya Jumamosi, Machi 22, 2025. Majengo mengine kadhaa muhimu yaliangukia mikononi mwa wanajeshi wa Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, ikiwa ni pamoja na Benki Kuu na Jumba la Makumbusho la Kitaifa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mafanikio ya kiishara yanakuja makubwa na ya haraka kwa Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan katika mji mkuu, ulioharibiwa na miaka miwili ya vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo ni vigumu kukadiria kwa usahihi idadi ya watu waliopoteza maisha.

Siku ya Jumamosi, msemaji wa jeshi la taifa, Jenerali Nabil Abdullah, alitangaza katika taarifa “mafanikio” ambayo yalipelekea kukamatwa tena kwa majengo kadhaa mjini Khartoum usiku wa kuamkia Jumamosi, ikiwa ni pamoja na Benki Kuu ya Sudan, makao makuu ya idara ya ujasusi na Makumbusho ya Kitaifa. Pia alisema jeshi “liliwaangamiza mamia ya wanamgambo waliojaribu kukimbia.” Taarifa ambayo ni vigumu haiwezekani kuthibitisha.

Vitongoji kadhaa bado viko mikononi mwa RSF

Kukamatwa kwa maje,go haya muhimu kunafuatia kukamatwa kwa ikulu ya rais siku moja kabla, na kuandamana, kama kawaida, na video za ushindi zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii. Katika wiki za hivi karibuni, jeshi la kitaifa limepata ushindi wa wazi katika mji mkuu, lakini maeneo kadhaa yamesalia mikononi mwa RSF ya mpinzani wake, Jenerali Hemedti.

Wakati huo huo, mapigano pia yanaendelea huko Darfur. Kulingana na wanaharakati wa mashirika ya kiraia, raia wasiopungua 45 waliuawa siku ya Alhamisi katika shambulio la kijeshi katika mji wa Al-Malha, Kaskazini mwa Darfur. Wanajeshi hao walidai kuuzingira na kuuteka mji huo na kuua zaidi ya maadui 380. Eneo kubwa la Darfur karibu lote liko chini ya udhibiti wa RSF, ambayo, hata hivyo, imeshindwa kukamata mji wa El-Facher.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *